Leo naomba tuangalie japo kwa uchache mambo matano ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha Success is a choice: make the choice that make you successful by John C. Maxwell.

1. Chagua kuwajibika: mwandishi maxwell anasema ya kwamba mafanikio huanzia kwa kuchukua umiliki wa maisha yako na kuchagua vitu sahihi. Vitu ambavyo ni chanya vitakavyokusaidia kwa namna moja ama nyingine kuwa chanya na kupata mafanikio. Acha kulamimika kwenye mambo yanayoendelea bali wajibika kwa kufanya maamuzi na kuchukua hatua sahihi zitakazokupa mafanikio chanya.

2. Kubali kukuwa kifikra: Maisha ni kujifunza, hivyo usione tabu ya kujifunza mambo chanya kila siku. Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu hiki anasema mtu anapojifunza kila siku inamsadia sana mtu huyo kuweza kuongeza kasi ya utendaji wa kazi zake, pia inakusaidia kuweza kutafakari mambo chanya ambayo yatakusaidia kufanya kazi kwa muendelezo bila kuchoka.

3. Shughulika na majibu na si matatizo: Jamii yetu mara nyingi hushughulika zaidi na matatizo badala ya kushugurika na kutafuta majibu ya tatizo hilo. Mwandishi wa kitabu hiki maxwell anasema kila wakati jifunze kutafuta majibu ya matatizo kwa kuangalia fursa kisha chukua hatua zitakazokusaidia kutimiza malengo yako.

4. Jenga mahusiano chanya na watu wengine: Kila wakati jifunze kujenga mahusiano chanya na watu wengine wanaokuzunguka. Jenga mahusiano chanya na watu ambao mnasapotiana kwenye mambo mbalimbali. Kitabu hiki kinatusisitiza sana kujenga mahusiano imara  yatakayokusaidia kukua na kutimiza mambo uliyojipangia kuyatimiza.

5. Chagua vitu vyenye thamani kwako: Si kila kitu ni lazima uwe nacho bali vitu vingine ni vya kuachana navyo. Ukishindwa kutokuwa mtu wa kuchugua vitu utayumbishwa na mambo mengi sana maana akili yako itashindwa kufanya maamuzi, hivyo jifunze kuchagua vitu ambavyo ni muhimu na vyenye thamani zaidi kwako, vitu hivyo ndivyo unavyopaswa kushughulika navyo.
Ukiyazingatia mambo hayo utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako. 

Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.