BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Nidhamu ni muhimu kwenye kila jambo ulifanyalo.

Kivyovyote vile kwenye kila jambo ambalo unalifanya kumbuka huwezi kuwa bora zaidi ya wengine, ila unaweza kuwa na nidhamu zaidi ya wengine wote kwenye kila jambo fulani unalolifanya. Kila kitu kinahitaji nidhamu ya hali ya juu katika kutekeleza jambo fulani.

Huwezi kusema unataka kufanikiwa katika jambo fulani wakati huo huo nidhamu haipo pamoja nawe katika kufanya jambo fulani, hapo utakuwa unajidanganya. Kumbuka kila kitu ili kiweze kuwa bora zaidi kinahitaji nidhamu ya hali ya juu katika kukamilisha hilo. 

Nidhamu ya kutenda jambo fulani kulingana na vile ulivyojipangia ni lazima ifuate mkondo wake kama kweli unataka kufanikiwa.

Kumbuka hakuna jambo litakalokutenga na umaskini kama  nidhamu, nidhamu ya kuliheshimu jambo husika na namna ya kulitenda jambo hilo  ni muhimu sana. 

Kwani kama  hautakuwa na nidhamu ya kutenda jambo fulani hapo utakuwa unajidanganya tu.  Nidhamu  ya muda katika kufanya jambo fulani, nidhamu ya namna ya kutumia muda wako katika kutenda yale yaliyo ya muhimu basi ni lazima yawe upande wako hapo ni lazima utafanikiwa.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments