Ukitaka kufanikiwa katika jambo fulani basi wataalam wa mambo wanasema unatakiwa kutafuta fursa zilizojificha ambazo zinafanywa na wachache, kwani kufanya hivyo watu wengi watataka kujua kwa undani juu ya kitu hicho na watu hao iwe au usiwe ni lazima watakupa pesa tu.
Ni muhimu kutafuta fursa zilizojificha kwa sababu huko ndiko siri ya utajiri ulipo. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika mambo fulani kwa sababu watu wengi wanafanya mambo yale yale ambayo yanafanywa na watu wengi na kwa wakati mmoja kwa kutumia mbinu zile zile za kila siku zinazofanana.
Iwe ni biashara au kitu chochote kile kumbuka kwamba ili uweze kufanya vizuri kupitia kitu hicho ni lazima utafute fursa iliyojificha (hidden opportunity). Fursa iliyojificha ni fursa ambayo wengi hawaijui, pindi wewe utakapoifanya watu waijue itakuwa ni fursa kwako kuweza kutengeneza kipato.
Mwingine ataniuliza nitaipata wapi hiyo fursa mpya, jibu lipo wazi kwamba; fursa mpya hupatikana kwa kutafuta maarifa yatakuongezea kitu katika akili yako, maarifa hayo yatakusaidia kupiga hatua katika maisha yako. Ni muhimu kutafuta maarifa ikiwa watu wengine wanatafuta vitu kwa ajili ya kuburudisha nafsi na mioyo yao. (kuwa mtu wa tofauti wa kutafuta maarifa chanya).
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments