Siku moja nilikuwa nasoma historia ya mianzi ya kichina, mianzi ya kichina huchukua takribani miaka mitano kuchipua toka siku uliyopanda mbegu ya mianzi hiyo. Hapo ndipo niligundua kwamba kumbe kuna baadhi ya mambo huchukua muda mrefu sana kabla mambo hayo hutujaona mafanikio yake.
Kama ilivyo kwa mianzi ya kichina katika mlolongo wa ukuaji wake hata wewe unapaswa kuelewa kwamba yapo baadhi ya mambo huchukua muda mwingi kabla mambo hayo hayajakuletea faida hivyo unapswa kuwa mvulimivu huku ukiongeza juhudi za maksudi katika kutenda jambo hilo.
Hivyo unapaswa kuwa mvulimivu huku ukiongeza juhudi katika kufanya jambo fulani wakati ukisubiria mafanikio hayo. Kumbuka vitu vikubwa huchukua muda ili viweze kuleta mafanikio, hivyo uvumilivu unapaswa kuchukua nafasi yake. Hakuna mafanikio ya muda mfupi.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments