BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze kutoa thamani itakayokulipa.

Kama unatoa thamani kwa watu wengine, hakikisha pia thamani hiyo inarudi kwako. Usiishie tu kuwasaidia watu wengine na hao watu wakabaki wanakuangalia. Ni muhimu na lazima sana thamani hiyo irudi kwako pia.

Kwa mfano, kama kazi yako ni kuandika, hakikisha unaandika na maandiko hayo kwa baadae yaje yakulipe iwe kwa watu kukulipa wewe moja kwa moja au kufanya mauzo ya vitabu vitakavyo kupa pesa.

Pia kama viwanda vya magari vingekuwa vinatoa magari yao bure, watu wangefurahi, lakini, ingefika muda viwanda hivyo vingefungwa kwa sababu, wafanya kazi wange acha kazi kwa kukosa malipo.

Hiyo maanake ni nini, kila thamani yoyote ile unayoitoa lazima irudi kwako na kama ikitokea isiporudi kuna sehemu kutakuwa na shida. Itafika muda thamani ile iliyokuwa ikitolewa mwanzo haitapatikana tena.

Kama unatoa thamani kwa watu wengine, hakikisha pia thamani hiyo inarudi kwako. Usiishie tu kuwasaidia watu wengine na hao watu wakabaki wanakuangalia. Ni muhimu na lazima sana thamani hiyo irudi kwako pia.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.

Post a Comment

0 Comments