Ili uweze kufanikiwa katika eneo lolote lile iwe ni kibiashara, maisha, mahusiano, uchumi au eneo lolote lile basi unatakiwa kutumia akili yako kuweza kufanya vyema katika jambo hilo. Au kwa maneno mengine unapaswa kuwaza nje ya box, yaani mawazo yako yawaze jambo katika kuongezea thamani katika eneo fulani.
Usiishie kuwaza jambo fulani katika udogo fulani, bali unatakiwa kuwaza jambo fulani katika mawanda makubwa. Kwa mfano kama unafanya biashara fulani kwa njia ya mazoea kaa chini kisha uwaze mbinu mpya ambayo itakusaidia kwa namna moja ama nyingine ni kwa namna gani unaweza kupata wateja wapya.
Kwa mfano leo hii kuna baadhi ya watu wamekuwa wakizichukulia takataka ambazo tunazitupa kwa ajili ya kutengeneza au kuzalisha bidhaa zingine. Kile ambacho unakiona kwako ni uchafu kwa watu wengine kwao ni fursa.
Huku ndiko kunakoitwa kuwaza nje ya box. Kuna wakati mwingine unapaswa kuwaza na kuona ni kwa namna gani kitu fulani kikakusaidia kuwa bora. Jifunze kutumia jicho la tatu kuona zaidi ya uonavyo kwa macho mawili.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments