Zipo hatua tatu za mafanikio yoyote yale unayoyatafuta kwenye maisha yako. Hatua hizo ni hatua ya mwisho, hatua ya mwanzo na hatua inayofuata. Hizi ni hatua za lazima na msingi sana kwako kuzijua.
Hatua ya mwisho, inakutaka uwe unajua kile unachokitaka, inakutaka uwe na picha kamili ya malengo yako unayoyataka. Kama huna picha kamili basi hapa ndio mwisho wako na hutaweza kufanikiwa.
Hatua ya kwanza, inakutaka wewe sasa kwenda kwenye vitendo au hatua. Inakutaka kupiga hatua za kuelekea kwenye mafanikio yako. Usipopiga hatua huwezi fanikiwa. Piga hatua.
Hatua inayofuata, hapa inakutaka kupiga hatua inayofuata ili kufanikiwa. Ni lazima upige hatua inayofuata hadi uweze kufikia malengo yako uliyoyaweka. Kila wakati unatakiwa kupiga hatua.
Hizo ndio hatua tatu muhimu za mafanikio yako unazotakiwa kuzijua na kuzifanyia kazi. Mafanikio yako yote yanaanzia kwenye hatua hizo tatu za msingi. Fanyia kazi kwa umakini kila hatua na utafanikiwa.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments