Kitabu "Excellent Advice for Living" kilichoandikwa na Kevin Kelly kinatoa ufahamu wa thamani kuhusu maisha na jinsi ya kuishi vizuri.
Leo nimekuletea mambo kumi muhimu ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hicho:
Ishi sasa: kwenye maisha haya tunakumbushwa kuishi sasa kwa sababu sasa ndiyo tunayoimiliki mikononi mwetu. Kuishi jana ni sawa na kupoteza muda, hivyo kama unataka kufanya jambo fulani lenye manufaa anza kulifanya leo. Mwandishi anatukumbusha kuzingatia na kuthamini wakati huu na kufurahia sasa badala ya kusubiri kwa ajili ya siku zijazo.
Kujifunza kutoka kwa wengine: kuna hekima katika kusikiliza na kujifunza kutoka kwa uzoefu na maoni ya wengine. Unapojifunza kutoka kwa watu wengine unapata ufahamu mpya ambao ulikuwa haujui hivyo, inakuwa rahisi zaidi kwako ule ufahamu unaoupata kutoka kwa watu wengine kuweza kuutumia kwenye mambo yako.
Kukubali mabadiliko: unapotaka kukua zaidi na zaidi kumbuka ni lazima utakutana na mabadiliko. Mabadiliko ni sehemu ya maisha, na kuwa tayari kuzoea na kukumbatia mabadiliko kunaweza kusaidia katika kukua. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa hasi au chanya hivyo jiandae kuyapokea mabadiliko yote ambayo yatatokea.
Kuwa na shukrani: Kushukuru kwa kile unachopata kunaweza kusaidia kukuza mtazamo chanya na kufurahia maisha zaidi. Mtu mwenye shukrani ndiye anafanikiwa zaidi. Huwezi kufanikiwa kama si mtu wa shukrani, mafanikio yatajitenga nawe. Jifunze kushukuru kwa kila kitu unachopata.
Endelea kujifunza: tupo duniani kwa lengo la kujifunza, hivyo ili tuweze kuwa bora zaidi tunapaswa kuendelea kujifunza na kukuza ujuzi ni njia muhimu ya kuboresha maisha yetu. Kujifunza hakuna ukomo hivyo yatupasa tuendelee kujifunza bila kuchoka.
Kuwajali Wengine: Kuonyesha huruma na kujali kwa wengine kunaweza kuunda uhusiano wenye thamani na kuleta furaha. Kila wakati unatakiwa kuwajali watu wengine kwa kuwasaidia katika kutatua shida zao. Shida hizo zinaweza kuwa ni za kifedha, malazi, chakula au hata muda mwingine msaada wa kimawazo. Msaada wowote unaoutoa ni baraka kwani unavyotoa ndiyo unazidi kubarikiwa zaidi.
Jifunze kufuata nia yako: kila mmoja wetu ana nia yake. Kufuata ndoto zako na kufanya kazi kuelekea malengo yako ni muhimu katika kupata furaha na mafanikio. Mwandishi anatutaka kuwa ni watu ambao tunatimiza nia zetu, kama nia yako ni kufanya jambo fulani basi hakikisha jambo hilo linakamilika kweli.
Jenga urafiki mzuri na wengine: usipende kuishi bila marafiki bali unapaswa kuwa na marafiki na uhusiano wa karibu kunaweza kuongeza furaha na kuleta msaada wakati wa changamoto. Pia kumbuka unapaswa kichagua marafiki wazuri ambao watakuwa na tija zaidi kwako.
Kutunza Afya: afya ni mtaji nambari moja, usipokuwa na afya imara kila kitu kwako kitakuwa hakiendi sawa. mwandishi anatuasa kujali afya yako kimwili na kisaikolojia ni muhimu katika kuishi maisha yenye furaha na mafanikio. Kula vyakula stahili, fanya mazoezi pia epuka mambo yatakayokuathiri kisaikolojia.
Kufurahia safari yako ya kimaisha: epuka kuishi kwenye makasiriko, bali jifunze kuishi kwa furaha zaidi huku ukifurahia kile unachokifanya. Kuishi kwenye makasiriko hupunguza morali wa utendaji wa kazi zako binafsi, si maoni yangu bali ni kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu hiki.
Kujifunza na kuzingatia miongozo hii kunaweza kusaidia katika kuboresha ubora wa maisha na kuleta furaha na mafanikio. Tafuta kitabu hiki ili usome mwenyewe mengineyo.
Imeandikwa ña Afisa Mipango Benson Chonya
0 Comments