Maisha yanatakiwa yaende kwa utaratibu, na sio kukimbia kimbia tu kusiko kwa msingi, kila kitu kinatakiwa kiende kwa utaratibu, hatua kwa hatua, na kwa umakini hadi kufanikiwa. Maisha ya mpangilio ni ya uhakika.
Kama vile ambavyo kila siku unahema kwa utaratibu na huwezi kuhema kwa ajili ya kesho, na maisha yako unatakiwa uyaendeshe hivyo hivyo hata kama ni kwa mwendo wa kobe ilimradi kila siku yanakuwa bora.
Hakuna aliyesema kuharakisha katika Maisha ndio utafanya maisha yako yawe bora. Unaweza ukaharakisha sana na ukajikuta umejiingiza kwenye shida kama kudhulumu na ukajiharibia zaidi ya mwanzo.
Siri ya kufanikiwa kwako, nenda pole pole utafanikiwa. Kama upo ulazima wa kwenda kasi, basi fanya hivyo lakini hakikisha usiwaumize wengine na pia hakikisha unafanikiwa na kufanya maisha yako kuwa bora.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments