Confucius anatukumbusha kwamba kila kitu kina uzuri wake lakini changamoto iliyopo siyo kwamba kila mtu anaweza kuona uzuri huo. Confucius alizungumza hayo hasa pale alipokuwa anazungumzia namna ya kuona fursa katika maeneo uliyopo.
Confucius anasema mara nyingi fursa zina tabia ya kujificha hivyo zinasubiri uzifuate, lakini kwenye suala la kuzifuata fursa hizo siyo wote ambao wataziona na kuzipenda. Anasema wengine wanaweza kuziona lakini wasizipende pia.
Pia anasema pindi utakapoona fursa ya aina fulani, na fursa hizo zina uwezo wa kukusogeza kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine basi acha kuzionea aibu fursa hizo bali unapaswa kuzifuata fursa hizo, kwani wewe ndiyo umeona uzuri wa fursa hizo.
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp, au
BONYEZA HAPA mafanikioapp@gmail.com kuwasiliana nasi kupitia email kwa
ajili ya Maoni, Ushauri, Mapendekezo au
Changamoto.
.png)
0 Comments