Je, ulishawahi kujiuliza ili upate bahati unatakiwa ufanyaje? Lipo jambo moja la kufanya kama unataka bahati, nalo ni kujituma tu. Ukiweza kujituma na kuweka bidii, bahati utaipata.
Jinsi unavyofanya kazi kwa juhudi, ndivyo unavyoongeza bahati yako. kama kuna bahati kwenye kazi na biashara basi inatokana na kujituma sana kwenye kile unachofanya.
Wale unaoona wana bahati, ni kwamba wanajituma kuliko wengine. Hakuna bahati ambayo inaweza ikakuta ukiwa umelala. Siri ya kupata bahati inatokana na wewe kujituma kwako.
Anza kujituma leo bila kuchoka, nakwambia bahati utaipata. Kila mtu ana uwezo wa kupata bahati ikiwa ataamua kujituma kweli katika kile akifanyacho. Jitume kwa nguvu, bahati utaipata.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments