Kama kuna kazi unaifanya iko mbele
yako, acha kuifikiria kwamba kazi hiyo ni ngumu, bali ifikirie kazi hiyo ni ya
muhimu unatakiwa kuifanya kwa umakini na usahihi mkubwa.
Unapojiwekea fikra ya kuwa kazi hiyo ni ngumu, itakuwa ngumu kweli kwako. Kila wakati toa mawazo kabisa, yanayosema kazi hii ni ngumu au majukumu hayo ni magumu sana kwako.
Ukiacha kufikiria hivyo kuwa kazi ni ngumu na ukaamua kuchukua hatua za kufanya kama kazi ya muhimu, basi utaweza kufanikisha kazi hiyo unayosema ni ngumu, tena kwa urahisi.
Badili
fikra zako, badili mtazamo wako, unaowaza kazi hii ni ngumu na kuwaza ni kazi
ya kawaida na muhimu inayoweza kufanyika bila tatizo kubwa kwako. Ifanye kazi
hiyo.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments