BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo la kujifunza kutoka kwa Euripides.



Euripedes aliwahi kusema ya kuwa hisia kubwa katika maisha ni upendo. Hivyo sisi kwa sisi tunapaswa kutekeleza hisia hizo kwa kupendana pasipo kuwa na chuki. Upendo ndiyo msingi wa mafanikio kwenye kila jambo. Kama tutatunguliza chuki za aina yeyote ile basi kufanikiwa kwetu kwenye jambo lolote lile itakuwa ni ndoto. 

Hata vitabu vya dini vinasisitiza sana kwamba tunapaswa kupendana, Upendo ndiyo amri mpya ambayo mwenyezi Mungu alitutaka tuishi ili tuweze kufanikiwa zaidi. Tukitanguliza upendo mbele kwenye kila jambo maisha yatakuwa ni mazuri kwa sababu hakutakuwa na roho mbaya zenye kutufanya turudishane nyuma.

Tunapaswa kuishi kwenye sayari ya upendo ili tuweze kuishi kwa furaha, tupendane ili tuweze kusaidiana mambo mbalimbali, tupendane ili tuweze kuinua kiuchumi, tupendane ili tuweze kupeana maarifa ya kutujenga, tupendane ili kila jambo liweze kwenda sawa, tupendane ili tulete hisia sahihi katika maisha yetu. TUPENDANE. 

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp, au BONYEZA HAPA mafanikioapp@gmail.com kuwasiliana nasi kupitia email kwa ajili ya Maoni, Ushauri, Mapendekezo au  Changamoto.


Post a Comment

0 Comments