Zipo kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia kile. Usipokuwa makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya kuweza kujiokoa na kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele. Simamia na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na utafanikiwa.
Wako rafiki katika mafanikio, Imani Ngwangwalu
dirayamafanikio@gmail.com

0 Comments