Siku hii ya wapendanao au Valentine's day ina historia ndefu sana. Kwa mujibu vya vyanzo mbalimbali ambavyo vimealeza juu ya historia hii, vyanzo hivyo vinasema:
Siku hii ya wapendanao huaziamishwa kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka. Asili ya siku ya siku hii wapendanao au "Valentine's Day" imetokana na St Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Claudis II.
Mtakatifu huyu vellentine ni miongoni mwa watakatifu ambao licha na kuendelea kuhubiri neno la Mungu, ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanapenda na kuupigania Ukristo, mtakatifu valentine alikuwa yupo tayari kwa lolote katika kupigania Ukristo kwa hali na mali.
Pamoja na uwepo wa Mtakatifu huyu vallentine, palikuwapo na mtu ambaye alifanikiwa kwa jina la claudis ambaye alipigana sana na mtakatifu vallentine. Claudis hakupendelea na vitendo ambavyo aliendelea kuvifanya mtakatifu vallentine.
Hivyo claudis akaamua kuanzisha jeshi ambalo lingempinga mfalme claudia kwa hali yetote ile kwa kile alichokifanya. Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake.
Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao. Kwani vijana hao waliamini pindi wangeingia kwenye vita wangeziacha familia zao.
Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha ili waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana. Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya familia zao.
Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri.
Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.
Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori".
Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.
Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine wako )
Valentine ilipofika tarehe 14 februari mwaka 269 AD akanyongwa.
Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda salamu za mapenzi.
Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.
Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ni ya kibiashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe nyekundu.
Lakini kama hiyo haitoshi siku hii ya vallentine imekuwa ikiazimishwa kinyume na matakwa yake, kwani wengi wetu hudhani ni siku ambayo ni kwa ajili ya wapenzi tu. Lakini ukweli haupo hivyo siku hii inamaanisha unaweza kunyosha upendo kwa mtu yeyote kama ni sehemu ya kusherekea siku hii.
Hivyo nikusihi ya kwamba uwe na mtazamo chanya juu ya usherekeaji wa siku hii ya wapendanao, lakini unaweza ukaitumia siku hii kwa kumjali yule ambaye unampenda ili ajihisi ni sehemu ya watu ambao wanapendwa.
Nakutakia siku njema ya siku hii ya valentine day, Mwenyezi Mungu akulinde na akubariki siku zote za maisha yako.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya

0 Comments