Kwa namna ya pekee tuchukue fursa hii kukushukuru sana kwa namna moja ama nyingine kwa kuwa nasi kwa kipindi chote cha siku 365 za mwaka uliopita.
Uongozi wa Mafanikio App Unakutakia heri nyingi sana ya mwaka mpya 2026 wewe na familia yako.
Jambo la muhimu zaidi kwako ni hili:
Fanya tathimini ya mambo ambayo umefanya mwaka 2025. Angalia ni mambo gani ambayo umekamilisha kisha andika na yale ambayo hujakamilisha kisha anza nayo mwaka 2026.
Angalia vikwazo mbalimbali ambavyo ni chanzo cha kukukwamisha kwenye mambo yako, kisha tafuta njia sahihi ili usirudie makosa yatakayokukwamisha mwaka 2026.
Nb: Kwa siku Kumi na nne kuanzia leo hatutapost somo lolote hapa, siku hizo kumi nne ni siku za kufanya tathimini ya mambo ambayo tumeyafanya mwaka uliopita, pia siku hizo zitakuwa ni siku za kupanga mipango ambayo tutakwenda kuitekeleza mwaka ujao.
Tunaomba na wewe utumie siku hizi kama sehemu ya kufanya tathimini na kupanga mipango ya mafanikio yako binafsi, kumbuka unapopanga mipango uandike na njia ya kutekeleza mipango hiyo.
Nikutakie heri tena ya mwaka 2026, mwaka ukawe wenye baraka na mafanikio tele ndani yake.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya!

0 Comments