BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Uhuru wa kweli unakuja kwa wewe kufanya kile kinachohitajika kufanyika. Kama kuna kitu kinahitajika kifanyike na usipokifanya, uhuru huo wa kweli utaukosa, kwa sababu kila wakati utakuwa unafikiri kitu hicho jinsi ya kukifanya.

Sasa hapa fikiri, ni mambo gani unayotakiwa kuyafanya, na kisha amua kuyafanya mambo hayo. Ukishindwa kuyafanya mambo hayo, kaa ukijua, unajinyima uhuru wa kweli maana utayafikiria mambo hayo kuyafanya kila wakati.

Fanya sasa kile unachotakiwa kukifanya, ili uwe na uhuru wa kweli. Naamini unakijua unachotakiwa kukifanya, sasa kwa hiari yako kifanye hicho kitu ili kikupe uhuru wa kweli na uweze kufanikiwa.


Post a Comment

0 Comments