BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Kama haufanyi makosa katika maisha, hiyo iko wazi ni kwamba wewe huchukui hatua. Nakwambia hivyo kwa sababu, kuchukua hatua ndio njia pekee ya kukufikisha wewe kwenye ndoto au malengo yako na kuchukua hatua kunakufanya tu lazima ukosee.

Kuna wakati tunakua tunajitahidi sana tusikosee, lakini kukosea ni lazima kama unachukua hatua. Na njia nzuri ya kupata uzoefu na kujua ni kipi ambacho hakifanyi kazi katika njia ya kufikia ndoto yako au malengo yako ni kukosea.

Watu wenye mafanikio siku zote huwa wanaangalia hatua zao za nyuma zilizopelekea wakakosea na kisha hujirekebisha na kufanya kwa ubora mkubwa zaidi. Uzoefu wa kukosea unakuwa unawapa nafasi nyingine na kufanya kwa mafanikio.

Kwa jinsi unavyozidi kuchukua hatua, utajifunza kulingana na matokeo ya hatua unazochukua, maana ukichukua hatua, tegemea matokeo, yanaweza yakawa kama unavyotaka au hata usivyotaka yaani kufanya makosa.

Unatakiwa ukumbuke jambo hili na kulizingatia, kama hufanyi makosa kwenye maisha yako, basi huchukui hatua na hutafanikiwa. Hapo ulipo NENDA NJE KACHUKUE HATUA, FANYA MAKOSA, JIFUNZE NA UTAFANIKIWA.


Post a Comment

0 Comments