Habari ya mwaka mpya2026 kwa mara nyingine tena, bila shaka u mzima wa afya tele na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu pamaja na team yangu nzima ya mafanikio app hatujambo sana, tunamshukuru Mwenyezi Mungu.
Kila ifikapo tarehe 15 ya mwezi kwanza huwa tunaadhimisha siku ambayo app hii tulianzisha rasmi. App hii imekuwa msaada kwa watu wengi sana, kwenye kujibu maswali mbalimbali ambayo huwakabili watu kwenye maisha yao.
Lakini pia app hii imekuwa msaada mkubwa kwenye kuwapa hamasa mbalimbali hasa wale ambao nafsi zao zimekuwa zikikataa tamaa mara kwa mara. App hii leo hii imetimiza miaka mitano toka kuanzishwa kwake.
Tumepata marafiki wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa ni watumiaji wazuri sana wa app hii. Tunawashukuru sana tena sana kuwa sehemu ya app kwani maandishi haya ni bure bila uwepo wako.
Tarifa Muhimu zaidi.
Pamoja na yote hayo tunapenda kukutaraifu kwamba kuanzia leo app hii ndiyo imefika mwisho wake, hatutapost tena kwa sababu app yetu imetolewa kwenye Playstore toka tarehe 14 mwezi huu.
Zipo sababu mbalimbali ambazo zimesababisha app hii kutolewa kwenye playstore, hivyo sad news ni kwamba leo hii ndiyo mwisho wa MAFANIKIO APP.
Kiukweli tunatamani sana kuendelea kuwa na app lakini kwa hivi sasa kuwa app mpya na kuiweka playstore ni ngumu sana tena sana kwa sababu kumewekwa sheria ngumu sana otherwise tupate mtu ambaye tayari ana account ya playstore ambayo ipo live playstore.
Itakumbukwa vyema miaka ya nyuma ilikuwa ni rahisi kununua account ya playstore na kisha ukatengeneza app zako na kuziweka playstore ila kwa sasa ni ngumu sana tena sana kununua account mpya.
Kutokana na ugumu huo, ndiyo sababu iliyotupelekea tusitishe kupost masomo tena hapa, kwa sababu hatuwezi kurudisha app tena playstore.
Najua fika huenda ni taarifa ambayo itakuwa imekushtua sana ila hatuna namna tena ndugu yetu, zaidi tunafikiria ndani ya siku kadhaa mbeleni tutahamia Youtube ambako huko tutaandaa makala nzuri kwa njia video na sauti na jina la channel yetu tutaiweka hapa pindi itakavyokuwa tayari ili uweze kusubscribe.
Tukushukuru sana kwa kuwa pamoja nasi kwa kipindi chote ila zaidi ya yote pole pia kwa changamoto hii kwani tunajua nawe imekuathiri kwa namna moja ama nyingine.
Asante na kila lenye kheri katika safari yako ya mafanikio.
Ni Mimi Afisa Mipango Benson Chonya.
0747-030303
0 Comments