Kama ukiishi kwa kuwa na mawazo ya jana, utajikuta una huzuni na hasira na pengine hata msongo wa mawazo. Hivyo vyote vinakuja kwa sababu unakuwa unaangalia, baadhi ya mambo ambayo hukuyakamilisha jana au ulikosea yanakua yanakuumiza sana.
Lakini kama ukiishi kwa kuwa na mawazo ya kesho, nayo hiyo utajikuta una wasiwasi na mashaka mengi. Kila wakati utakuwa unajiuliza jambo lile kesho litakuwaje kama sitalifanikisha na nitafanyaje, mwisho unajikuta uko kwenye mashaka makubwa na wasiwasi.
Dawa ya yote hayo ni kuamua kuishi kwa kuwa na mawazo ya leo au sasa. Kama ukiishi leo amani na furaha utakuwa navyo maishani mwako. Amua kuishi sasa na achana na habari za kuishi jana au kesho zitakuhuzunisha tu.

0 Comments