BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Chochote unachokizingatia katika maisha yako ni lazima kitanuke na kukua. Haijalishi kitu hicho ni kizuri au kibaya, ukikizingatia, utakipata.

Kama unazingatia matatizo na akili yako kila muda ikawa hapo kwenye kuwaza matatizo, lazima ukae ukajua matatizo hayo yatakua makubwa siku hadi siku.

Kama unazingatia hofu, elewa hofu hizo zitakua na kuwa kubwa mpaka kushindwa kufanya kitu, maana hicho ndicho unachokizingatia.

Mawazo yetu yana nguvu sana. Kwa chochote kile unachokizingatia mawazo yetu yana uwezo wa kutupa kitu hicho kwa uhakika na asilimia zote.

Kuwa mwangalifu na unachokizingatia maana ni rahisi kukikuza na kukipata. Kila wakati waza mawazo chanya na ukiwaza hivyo, utafanikiwa.


Post a Comment

0 Comments