BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Kila wakati kataa kuwa na mawazo, ya kufikiria mambo ambayo huna, kama vile pesa, nyumba, au gari. Kama unafikiria sana vitu ambavyo huna unajiumiza tu bure.

Unatakiwa ufikiri vipi sasa, badala yake, fikiria yale mambo yale ambayo unayataka uyapate maishani mwako. Kama ni pesa, nyumba au gari, waza utapataje na sio kujilaumu kwa nini huna.

Kama unakazana kufikiria mambo ambayo huyataki au huna na unajilaumu kwa nini huna, nakwambia hayo mambo utayapata tu hata kama huyataki, kwa sababu unayafikiria.

Shukuru kwa mazuri na vile vitu ulivyonavyo, na kisha weka nguvu zako kufikiri juu ya mambo ambayo unayataka yatokee kwenye maisha yako si kifikiria fikiria mambo ambayo huna.


Post a Comment

0 Comments