BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Chochote kile unachokitaka, kina changamoto zake. Usijadanganye kwamba changamoto hakuna, changamoto zipo na tena nyingi tu, kwa chochote ukitakacho.

Kitu unachotakiwa kufanya ili kupata hicho unachokitaka na kuleta mabadiliko, ni kujitoa na kuamini kuwa una uwezo wa kushinda changamoto.

Hata kama maisha yako hovyo, bado una uwezo wa kufanikiwa. Hakuna kinachoshindikana kwako kama kweli ukiamua kupambana, utaweza.

Unatakiwa kujipa moyo wa kuweza hata kama mambo yanakatisha tamaa. Kwa kuwa na moyo huo utaweza kupambana na jambo lolote na utashinda.


Post a Comment

0 Comments