Haijalishi malengo yako yana changamoto kubwa kiasi gani ili kuweza kuyafikia, ila, kama utajipa nafasi ya ubunifu, basi, malengo hayo utayafikia kwa haraka kinyume na unavyotegemea.
Watu wengi ni watumwa wa kufanya mambo yao kwa namna ile ile, siku hadi siku, miaka na miaka. Na wanafanya hivyo kwa sababu wamezoea, matokeo yake hujikuta wakifanya mambo yale yale, bila mafanikio makubwa sana.
Unatakiwa kuelewa, haitumii nguvu nyingi kuwa mbunifu au kufanya malengo yako kwa njia ya utofauti. Unatakiwa ujue jinsi ya kufanya malengo yako kwa njia tofauti tofauti ili uweze kufanikiwa.
Inatumika nguvu ile ile kufanya kazi hiyo iwe kwa ubunifu au sio kwa ubunifu. Kama iko hivyo, amua kuwa mbunifu ili uyafikie malengo yako kwa haraka sana. Tuliza mawazo yako na kuwa mbunifu, utafanikiwa sana.

0 Comments