BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Mafanikio sio kitu ambacho unaweza ukatoka nje na kukipata. Ipo kazi ya kufanya ili upate mafanikio na mafanikio hayaji kiholela tu, unatakiwa uvute mafanikio yako kama sumaku inavyovuta chuma.

Kwa mfano, ikiwa unataka kuvuta watu wenye nguvu waje kwako, lazima uwe na nguvu. Ikiwa unataka kuvuta watu wabunifu uwe karibu nao, lazima uwe mbunifu pia. Unaona, ili uvute kitu, mvuto kwako ni lazima.

Tambua, hakuna mtu atakayevutiwa na wewe kama huna kitu cha kuwavuta ili waje kwako. Ni lazima wewe uwe kama hao watu na ndio nao watakuja kwako vivyo hivyo, kinyume cha hapo, unajidanganya.

Dunia ina watu wenye mipango mizuri sana, lakini hakuna anayejali mipango au ndoto zako, hata ziwe nzuri sana. Kuchukua hatua ndio msingi wa mafanikio yako, vitendo vina sauti kuliko unachoongea bila hatua.

Jambo kubwa zaidi ambalo unatakiwa uelewe, ikiwa unataka ulimwengu ukupe thamani na utajiri, basi lazima uwe mtu wa thamani. Yale mambo unayoyataka ni lazima uwe nayo kwanza wewe mwenyewe.

Kama ikiwa hivyo, yaani ukawa mtu wa thamani, mambo hayo unayoyataka yatakuja kwako bila pingamizi. Hivyo ndivyo mafanikio yanavyovutwa kama sumaku. Anza kuwa sumaku ya mafanikio yako.


Post a Comment

0 Comments