Kama unajua kweli kile unachokitaka kwenye maisha yako, basi utatumia muda mwingi kukifanya kitu hicho. Na kama hujui unachokitaka kwenye maisha yako, pia basi utaishia tu kutimiza ndoto za watu wengine.
Kama unaishi kwa kutimiza ndoto za watu wengine, acha kulalamika, chochote watakachokifanya juu yako na hutakiwi kuwalaumu. Kama wewe hujui unachokitaka, acha watu wakutumie.
Uamuzi unabaki kuwa kwako kuchagua, kujua kile unachokitaka au kutokukijua. Na ikitokea hujakijua basi tambua utatumikishwa na wengine maisha yako yote na utakuwa huna mtu wa kumlaumu.
Zipo chaguzi mbili za kufanya, chagua kile unachokitaka uwe huru, au chagua kile usichokitaka utumikishwe, uchaguzi unabaki kwako unataka nini kati ya hivyo vitu viwili na hakuna mtu wa kukulazimisha juu ya hilo.

0 Comments