BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Maisha safi na bora yanakuja kutokana na uzoefu wa wewe kuendelea kujifunza kila siku. Jitoe kamwe kutokuacha kujifunza, na utaishi maisha bora na yenye kuridhisha sana.

Wakati tunasoma tulikuwa tuna walimu wa kutufundisha - ili kujifunza. Na kuna walimu wengi bora ambao kweli walijitolea maisha yao kufundisha na kuelimisha wengine.

Hata hivyo, mwalimu bora katika maisha yako ni WEWE. Maisha daima yanakuonyesha uzoefu wa kujifunza. Unaweza kuchagua kujifunza kutoka kwenye maisha au ukaacha. Yote yako katika mtazamo au uchaguzi wako. Kila kitu kinachotokea kwako, kiwe "kizuri" au kiwe "kibaya" ni fursa ya kujifunza.

Unapokutana na changamoto za kukurudisha nyuma, unakuwa na machaguo mawili.  Unaweza kuchagua kuwa na hasira na kinyongo juu yake, au unaweza kuchagua kujifunza kutokana na kushindwa huko. 

Unapochagua kujifunza kutokana na makosa pamoja na uzoefu, hapo unakuwa unaboresha maisha yako. Maisha yako yanakupa somo kwako kila siku la kujifunza. Ni juu yako kuamua kujifunza au kuacha. 

Unatakiwa kikubwa uelewe, maisha ndio mwalimu bora, jifunze kutokana na uzoefu unaokutana nao, watu unaokutana nao na mawazo mapya unayokutana nayo na hapo utafanikiwa sana.


Post a Comment

0 Comments