Watu wengi wako bize sana kwenye maisha yao. Ukiwaangalia kwa nje na kwa haraka utaona ni watu ambao wako bize sana na shughuli zao, ambazo zinawapa faida.
Pamoja na kwamba watu hao wako bize hilo halina shida sana. Lakini, cha kujiuliza watu hao wako bize na nini? Hicho kinachowaweka bize kinawapa mafanikio watakayo?
Utakuta watu wengi wako bize kweli, lakini bado ni watumwa kwa kufanya mambo kwa mfumo ule ule, matokeo yake maisha yao yanabaki kama yalivyo hapo kwa miaka mingi, bila mabadiliko.
Ni muhimu ukawa bize, lakini ni muhimu kukumbuka pia kubadili utendaji wako wa kazi ili ufanikiwe, la sivyo utabaki hapo ulipo kwa miaka mingi sana bila mabadiliko makubwa.

0 Comments