Kama unaendelea kutimiza ndoto za mtu mwingine na kusahau zako, naomba nikukumbushe tu, maisha ni mfupi sana na unayo maisha ya kuishi mara moja tu.
Ni jukumu lako kuamua kupambana na kuachana na habari za kutaka kutimiza ndoto za wengine na kusahau ndoto zako ambazo ni muhimu.
Kufikia maisha mazuri sio rahisi, kunataka ujikane kwa mambo mengi na kuweka juhudi. Unatakiwa ufanye hivyo ili kufanikiwa, la sivyo, utashindwa.
Wakati wa kuishi maisha ya ndoto zako ni sasa, acha kusubiri kesho au wakati mwingine. Siku zinakwenda, unatakiwa kubadili maisha yako kwa wakati sahihi.

0 Comments