Kwa chochote kile unachotaka kufanya, amua kukifanya kidogo kidogo, pasipo kutumia nguvu nyingi, lakini fanya kila siku, kwa mwendo huo wa kidogo kidogo.
Kama ni kuweka akiba, anza kuweka akiba kidogo kidogo, mwisho wa siku akiba hiyo itakuwa kubwa kwako, lakini mwanzo wa yote ulianza kidogo kidogo.
Kama ni kutatua tatizo anza kulitatua pia kidogo kidogo. Chochote kile amua kukifanya kwa kidogo yaani 'less is more' na ukifanya hivyo utapiga hatua sana ya mafanikio yako.

0 Comments