Zawadi kubwa ambayo kila mtu amepewa ni UHAI. Kwa sababu tu, uko hai, amua kuishi kwa kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na wengine pia.
Pia kwa sababu unaishi, amua KUJIFUNZA. Maisha yako yatawaliwe na kujifunza hiyo itakusaidia sana katika kubadili pia maisha yako na wengine.
Usiishie hapo tu kujifunza, kwa kuwa bado unaishi, amua pia KUKUA. Kua kiakili, kila siku uwe na mtu wa kukua na ili ikusaidie kubadili maisha yako, usipokua, utakwama.
Lakini pia, VUMBUA. Hapa naweza nikasema uwe mbunifu. Usiishie tu kuishi kizembe uwe mbunifu na mvumbuzi kwenye kazi unayofanya.
Mwisho, kwa kuwa bado unaishi, FANIKISHA. Ifike muda unafanikisha yote ambayo umejiwekea kwenye malengo makuu ya maisha yako.
Kumbuka ndio maana tunasema na kusisitiza ishi, jifunze, kua, vumbua na fanikiwa (Live, learn, grow, create and achieve)

0 Comments