Kuwa na mawazo mazuri, lakini mawazo hayo huyafanyii kazi, hiyo ni sawa na kazi bure. Hakikisha uwe na mawazo bora na tena yafanyie kazi na yalete mabadiliko kwako.
Watu wanaofanikiwa hawaishii tu kuwa na mawazo bora, bali wanakuwa na mawazo bora, lakini pia wanachukua hatua kutokana na mawazo yao.
Kama unataka kubaki maskini, endelea kuwa na mawazo bora na kisha usiyafanyie kazi, uone kitakachotokea kama si umaskini wa kutupwa.
Siri ya mafanikio yako ipo kwenye mawazo bora, na kuchukua hatua, iko hivyo tu na hakuna cha ziada.

0 Comments