Matokeo makubwa na ya kushangaza katika maisha hayaji kwa bahati mbaya, bali yanakuja kwa kuweka vipaumbele vilivyowazi kwako. Hakuna utakachokipata kikubwa kwenye maisha yako, kama huna VIPAUMBELE.
Unapoishi bila vipaumbele hiyo ni sawa na kwako wewe kuamua kufukuza sungura wawili kwa wakati mmoja. Endapo ikitokea sungura hao wakipita kila mmoja na njia yake basi ni rahisi tu, hutampata hata mmoja.
Na maisha ulionayo yako hivyo hivyo pia, ni maisha yanayokutaka uwe na vipaumbele ni kipi unachokitaka. Kila wakati ili ufanikiwe, unatakiwa uchague vipaumbele vilivyo vya muhimu kwako na kisha vitekeleze.
Kinyume cha hapo utakuwa ni mtu wa kukimbizana kwenye maisha na kupishana na kila aina ya fursa na hakuna mafanikio ambayo utakuwa unayapata ya maana. Lakini kosa kubwa, linaanzia kwenye vipaumbele vyako.

0 Comments