Juzi kati nilisafiri kuelekea mkoani Njombe, nilipofika mkoa wa Iringa nilitafuta usafiri wa kuelekea huko mkoani Njombe. Nilibahatika kupanda gari aina ya (dungu) sijui kama ni kiswahili fasaha🤣.
Basi bwana ndani ya gari nikaona wameandika free WI-FI kwa chini wakandika password za Wi-Fi hiyo, kichwani mwangu nikawaza hawa watakuwa waongo, kwa sababu gari za dizaini hiyo kukuta ndani kuna huduma hiyo ni uongo.
Tuliendelea na safari, tulipozikata kama 40km hivi kutoka tulipoanzia safari, kondakta akatangaza, ndugu abairia asanteni sana kwa kuchugua kusafiri na gari letu, kwa wale wenye simu janja yaani smart phone tuna huduma ya bure ya internet ndani ya gari yetu, kisha kondakta ukataja tena password.
Afisa mipango, chap nikazama mfukoni na kutoka simu yangu na Headphone kisha nikaandika password kweli bwana kulikuwamo na huduma hiyo Wi-fi kwenye gari lile.
Nilifurahi sana na moyo wangu ulitabasamu kwa sababu sijawahi ona huduma hiyo kwenye aina hiyo ya gari. Safari iliendelea huku nikiendelea kuperuzi mpaka nilipofika Njombe....huduma ilikuwa kasi na pale mchawi ilikuwa ni chaji kuisha tu.
Tulipofika nilifuata kodakta na kumpongeza kwa huduma hiyo, kwani iliongeza thamani ya huduma wanayoitoa kwa abairia wake.
Ninachotaka kusema;
Ni hiki kwenye kile unachokifanya basi fanya kitu kingine cha ziada ambacho kitaongeza kitu kwa wateja, ambapo wateja hao watakuwa wanakukumbuka kila wakati na kila wakiwaza au kuhitaji kitu fulani basi mteja akufikirie wewe.
Ubunifu ni kitu chenye tija sana, hivyo kila wakati kuweka kitu chenye ubunifu kwenye kila huduma ambayo unaitoa kutakuongezea wateja. Tafuta utofauti ili kuwe na utofauti kati ya mtoa huduma A na mtoa huduma B.
Mmliki wa ile gari angekuwa amenilipa ningeitaja kampuni yake😃. Kwa kuwa lengo si kutaja kampuni lengo ni kuwa na wewe ujifunze jambo.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, ukiniita Afisa Mipango Benson Chonya, nitaitika.
0 Comments