Rasilimali tatu muhimu ambazo unatakiwa kuzitumia vizuri sana ili ufanikiwe ni muda, nguvu na pesa. Hizi ni rasimali ambazo kila wakati unatakiwa uzichunge sana kila unapozitumia.
Kama unataka kujua kitu unachokifanya hakina faida angalia tu, kitu hicho kinakupotezea muda, nguvu au pesa zako? Kama kitu unachokifanya kinakupotezea moja ya vitu hivyo vitatu au zaidi basi elewa hakiwezi kukufanikisha.
0 Comments