BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Najua katika maisha yako kuna watu wanakwambia huwezi kufanikiwa wala hutafika mbali kwa hicho unachokifanya, ukisikia hivyo usipate hasira wala usibishane nao, chapa kazi kwa bidii zote na waonyeshe kwamba inawezekana.

Najua tena watu wengine wanakwambia wewe si lolote wala si chochote na wanakubeza kwa kila namna, pia inapotokea hali hiyo katika maisha yako, usilalamike sana wala kuumia wape muda na waonyeshe jinsi inavyowezekana.

Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuamua maisha yako zaidi yako wewe. Hata dunia nzima iseme hauwezi jambo fulani, ukisimama imara na kuamua inawezekana, uwe na uhakika itawezekana kweli na utafikia mafanikio makubwa hata ubezwe vipi.

Sasa jiulize, kipi kinakusikitisha? Kipi kinakukwamisha? maneno ya watu? songa mbele, acha waseme watakavyo, wewe chapa kazi, lakini apa moyoni “I WILL SHOW YOU”. Ukiweka nia hiyo na ukapambana vya kutosha UTAFANIKIWA. 


Post a Comment

0 Comments