BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Kuna vitu au mambo ambayo kuna wakati fulani katika maisha yako ulishawahi kujiambia kwamba mambo hayo huyawezi tena, lakini leo nataka ufute hiyo kauli na kuamini kwamba hukuwa sahihi.

Nyakati katika maisha zinabadilika, fursa mpya kila siku zinazaliwa, kama kuna jambo ulijiambia huliwezi kabisa, upo uwezekanapo wa kuliweza sasa, kikubwa angalia tu jinsi ya kulifanya upya.

Acha kujiendelea kujifunga na maneno yako ambayo yanakurudisha nyuma, wakati wako wa kubadilika ni sasa na kutumia kila aina ya fursa inayokuja mbele yako hadi ufanikiwe.

Usiendelee kuamini tena katika kutokuweza ambako ulikuwa umeamini kwa muda mrefu. Leo hii unaweza tena kufanikiwa kwa sababu mambo na wakati umebadilika tena kwa kiasi kikubwa.


Post a Comment

0 Comments