Tunaambiwa hivi...ipo gharama ya kupata kile unachokihitaji katika maisha yako. Hili liko wazi na linaeleweka kabisa kwamba huwezi kupata kitu chochote mpaka ulipie gharama za aina fulani.
Kwa hiyo unaona wengi wanashindwa kufanikiwa si kwa sababu hawana uwezo bali ni kwa sababu ya kushindwa kulipa gharama za mafanikio yao. Hapo ndipo kushindwa kwingi kunapoanzia.
Kitu wasichokijua watu hao ni kwamba gharama ya kushindwa kulipa gharama hizo zinakuwa ni kubwa sana kuliko ambapo wangelipa gharama hizo ambazo zingewafikisha kufikia mafanikio yao.
Kwa mfano, ipo gharama kubwa ya kutokufanya kitu kuliko kufanya, gharama ya kutofanya ni mbaya mno kuliko gharama ya kufanya, gharama ya kutokufanya itachukua maisha yako yote yaani utakuwa mtu wa kushindwa tu.
Mpaka hapo unaona maumivu ya kushindwa kulipa gharama yanakuwa makubwa na ya muda mrefu sana kuliko maumivu ya kulipa gharama. Chagua kulipa gharama za kile unachokitaka ili ujenge mafanikio yako makubwa.
0 Comments