Kama kuna malengo umejiwekea na unataka uyafikie, lakini kila ukifikiria unaona malengo hayo ni makubwa sana kama hayafikiki hivi, kitu cha kufanya kwanza ili uyafikie malengo hayo, acha kufikiria ukubwa wa malengo hayo, badala yake fikiria jinsi utakavyoanza kutekeleza malengo hayo.
Fikiria pale utakapoweka miguu yako kwa mara ya kwanza ili uanze utekelezaji wa malengo yako. Tafuta jinsi utakavyoanza kwanza. Kumbuka hata safari yoyote ndefu inaanza na hatua moja, hata malengo yako ili yatimie, litafute eneo utakaloweka miguu yako kwanza, na kisha kuendelea na utekelezaji.
0 Comments