BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 

Fanya kila ufanyalo, lakini jitahidi sana usiwe msikindikizaji katika maisha yako. Kuwa makini sana na maisha yako, kuliko kitu chochote. Lakini kama utaendeleza vile vijitabia vidogo vidogo vya kushabikia maisha ya wengne na kujifanya na wewe unatafuta mafanikio. Unajidanganya sahau mafanikio ITABAKI STORI.

 Mafanikio hayaji eti kwa sbabu upo kwenye magroup 20 ya whats app au kwa sababu unajua fursa nyingi. Mafanikio yanakuja kwa kuchukua HATUA katika zile fursa hata kama hatua hizo ni kidogo. Unafikiri natania, endelea kucheza na maisha yako, utakuja kujuta na kuona mwenyewe baada ya miaka kumi kuanzia leo, utaelewa ni kitu gani kitatokea.

Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara si kila kitu kinaleta matokeo ya papo kwa hapo. Unachezea maisha yako leo sawa, zinatokea fursa unajishau kama ambavyo asemavyo rafiki yangi Meshack Maganga sawa, lakini ipo siku muda utasema tu, utajuta mpaka kwa nini ulikuwa unapoteza muda wako kuchati hovyo.

Maisha ni shule ambayo inataka nidhamu ya hali juu sana ili kuweza kufanikiwa. Vinginevyo ukizidi kuleta ile hali ya ‘utoto,’ au hali ya vijitabia vya ‘uchuo uchuo’ kwenye maisha yako umepotea. Kwenye maisha hatuigizi eti, maisha yapo ‘live.’ Kaa chini na tafakari mienendo yako iko sawa. Kisha chukua hatua.


Post a Comment

0 Comments