Habari, bila shaka u mzima wa afya tele? Kwa upande wetu sisi ni wazima wa afya tele, tunamshukuru Mungu hatujambo kabisa.
Kila ifikapo tarehe 19 ya mwezi wa kwanza basi huwa tunafurahia mwaka wa kuanzishwa kwa app hii ya mafanikio, na leo tunatimiza miaka minne toka tuanzishe app hii kwani ilianzishwa mwaka 2021.
Tunayofuraha kwani app hii imekuwa ni msaada mkubwa sana kwa wasomaji wetu kwani wengi wao hukiri wazi juu ya jambo hilo kwani imewafanya wazidi kufunguka kifikra kila wakati, jambo hilo linazidi kutufanya tuzidi kuandaa mambo mazuri zaidi.
Hatuna mengi ya kusema zaidi ya kusema asanteni sana, tukutakie mafanikio mema katika mipango yako kwa mwaka 2025.
0 Comments