Mafanikio makubwa yanakuja kwa wewe kuamua kufanya kwa ziada yaani, a little something more.'Usikubali kuishia tu pale unapoishiaga, unatakiwa kwenda hatua ya ziada kidogo. Mafanikio makubwa, yapo kwenye hatua ya ziada.
Waangalie washindi katika riadha, huwa wanashinda ushindi wao kwa sekunde chache tu au wakati mwingine wanashinda kwa nukta. Ukijua siri ya kufanya 'a little something more' wakati wote utabaki au utakuwa mshindi.
Nimekwambia, hata siku moja, usikubali kuishia pale unapoishia tu kila siku, ongeza juhudi kidogo, ongeza jitihada kidogo na juhudi hizo zitakupa ushindi mkubwa kuliko unavyofikiria. Usipuuze hili, fanyia kazi, utaona mafanikio yake.
Imani Ngwangwalu.
0 Comments