BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafaniko ya leo.




Utakuwa ni uongo mkubwa sana kama utajiambia kila unachofanya lazima kifanikiwe, sio kweli. Kwenye kuelekea mafanikio yako, tambua kuna changamoto na unatakiwa ukabiliane nazo.

Kila unachokifanya, elewa mbele kuna kizuizi au changamoto. Unatakiwa kukabiliana na vizuizi hivyo ili kufanikiwa. Kuwa mwepesi kujifunza kutokana na vizuizi hivyo, kisha songa mbele kwa ujasiri mkubwa.
Hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuwa mshindi katika kila anachokifanya. Hapa njiani kuna kushindwa sana. Unachotakiwa kufanya, usikubali kwa namna yoyote kusimamishwa na kushindwa kwako.

Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments