Natambua wewe hapo ulipo una matumaini, matamanio na ndoto za kufikia malengo yako, hata hivyo hiyo haitoshi, ili uweze kufikia malengo yako, unahitajika kuchukua hatua, tena kuchukua hatua kila siku bila kuacha.
Ikiwa kama hutachukua hatua, hata uwe na matamanio au uwe na kiu kubwa sana kiasi gani ya kufikia mafanikio yako, elewa na amini hutaweza kuyafikia hayo, zaidi ungeweza kushindwa, kama ambavyo unavyoshindwa.
Kumbuka kila wakati kwenye maisha yako, matumaini yako, ndoto zako, na shauku yako ya mafanikio, ni lazima viendane na wewe kuchukua hatua na hapo utaweza kifanikiwa, kinyume cha hapo sahau mafanikio.
Imani Ngwangwalu.
0 Comments