Unapokuwa na picha kamili ya kule unakotaka kwenda kimafanikio, na kisha ukaamua kujitoa kweli kufika huko, basi elewa hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kukuzuia tena, kufanikiwa huko.
Narudia, hakuna kitakachokuzuia kufika kule unakotaka kufika ukiwa na picha kamili ya malengo yako. Wale wote wanaokwama kwa sababu ya vizuizi, elewa ni watu ambao hawana picha kamili ya kule waendako.
Una nguvu kubwa ya kufanya chochote kile unachotaka kukifanya maishani mwako. Kikubwa, weka nguvu za uzingativu, jitoe na kuwa na picha kamili, amini utazifikia ndoto zako, bila tabu yoyote.
Imani Ngwangwalu.
0 Comments