BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo


Kwenye maisha yako, acha kutumia nguvu zako nyingi kwenye mambo hasi. Kama, ukitumia nguvu zako nyingi kwenye mambo hasi, basi elewa hivi, utakuwa unajichelewesha mwenyewe kuweza kufanikiwa.

Jitahidi sana kutumia nguvu zako na akili zako kwenye mambo chanya na sahihi. Ikitokea kinyume cha hapo, unajiharibia wewe, kwani nguvu hizo hizo, ndizo zingekusaidia kufanikiwa pengine kwa kiasi kikubwa.

Ni wajibu wako kila siku, na kila wakati kujiuliza, je, nguvu zako za mwili unazitumia katika mazingira sahihi au unazitumia katika mazingira ambayo kwako sio sahihi na yanakupotezea nguvu zako bure tu.

Imani Ngwangwalu

Post a Comment

0 Comments