BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo


Ili tuweze kupata vile tunavyovitaka kwenye maisha yetu, lilokubwa kwetu, tunatakiwa kuwa WAVUMILIVU tena kwa kiasi kikubwa.  Si kila kitu tutavipata kwa urahisi, uvumilivu pia unahitajika.

Mara nyingi vitu vingi ambavyo tunavitaka kwenye maisha, vimejificha kwenye upande wa pili wa ugumu au upinzani. Lazima kuna kupambana na changamoto ili kupata kitu hicho ukitakacho maishani mwako.

Tunapokuwa wavumilivu, hiyo ina maana uvumilivu unatusaidia kufikia malengo yetu. Kama tusipokuwa wavumilivu, ni wazi hatuwezi kufanikiwa. Wanaoshindwa ni watu, ambao hawawezi kuvumilia.

Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments