BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.


Mafanikio hayaji kama ajali. Mafanikio hayashuki tu kutoka angani na kutua chini. Inachukua muda, uzingativu na kujitoa ili kufanikiwa. Ni muhimu kujua kule unakotaka kwenda, na nini unachokwenda kufanya.

Jitahidi sana uwezavyo, ufanye mafanikio yako yaonekane kwako kwa wewe kuamua kujituma na kujenga nidhamu kila siku. Kama utakuwa huna nidhamu hiyo na pia huna ule  ung'anganizi, basi sahau kufanikiwa.

Waangalie watu waliofanikiwa, wote wamejitoa, wote wana nidhamu na wote wanaweka juhudi katika kufanikiwa kwao. Kama ukiona mtu hajajitoa, na mtu huyo hana nidhamu, basi mwisho wake ni kushindwa.

Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments