BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo



Watu wenye mafanikio, wanajisukuma wenyewe kuelekea kule wanakotaka kufika kimafanikio, lakini cha ajabu watu wengi, hasa wanaoshindwa, wao  wanasubiria kusukumwa kuelekea kwenye mafanikio yao.

Unapojisukuma mwenyewe kutafuta mafanikio, itafika muda utafika tu pale unapotaka, lakini ukisukumwa ni rahisi kwenda hata usipokutaka, kwa sababu unakuwa hujui kipi unakitaka, unakuwa umejiendea tu.
Ndani yako unatakiwa ukumbuke una fursa, matamanio na kiu juu ya mafanikio. Haya yote yatatimia kwa wewe kuamua kujisukuma katika kuchukua hatua na si kusukumwa. Ukisukumwa tu utapoteza mwelekeo.

Imani Ngwangwalu.

Post a Comment

0 Comments