Kitabu cha "Zero to One" kilichoandikwa na Peter Thiel ni chanzo kizuri cha maarifa katika ujasiriamali na uvumbuzi.
Hapa kuna mambo kumi ya kujifunza kutoka kwake:
1. Jitofautishe na wengine: Mwandishi anasema badala ya kuendelea kuboresha vitu ambavyo vipo basi wewe lenga kuunda kitu kipya ambacho hakipo sokoni. Kwenye hilo pia mwandishi anasema si lazima kiwe kitu kipya pekee bali hata mawazo na namna ya kufanya fulani ni lazima yawe ya tofauti ili yakutofautishe baina yako na wengine.
2. Kuwa mwaminifu: Mwandimamboshi Thiel anasisitiza kuwa ili uweze kushinda soko lako kikamilifu inabidi uweze kuwa mwaminifu kwa wateja wako. Uaminifu ndiyo utakaokuleta wateja wengi sana, badala ya kuendelea kushindana na wengine kwenye suala la bei basi wewe jitofautishe kwa kuwa ni mtu mwaminifu kwenye biashara yako ili uweze kupata wateja wengi zaidi.
3. Kuwa mbunifu: Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako ni lazima uweze kuwa na ubunifu, biashara yeyote ili ikue zaidi inahitaji ubunifu na ubunifu huo ni lazima kila wakati uandike makosa yako, na makosa hayo yaanze kuboresha ili viwe ni vitu sahihi. Maboresho madogo madogo ya kila siku ndiyo yatakayokufanya uwe na ubunifu kwenye biashara yako.
4. Kuwa wa kipekee: Mwandishi anasema kuwa ifanye bidhaa au huduma yako kuwa na kipekee sana kiasi kwamba kuwe hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya kama wewe. Kuendelea kufanya yale yale ya kila siku uliyoyazoea kuyafanya yatakufanya kuyapata matokeo yale yale uliyozoea kuyapata, hivyo tafuta upekee wako ili upate matokeo ya tofauti.
5. Fanya kazi na watu tofauti: jifunze kufanya kazi na watu tofauti tofauti kwenye biashara yako. Jenga timu ya watu wenye uelewa tofauti tofauti ili uweze kupata mafanikio yako. Unapofanya kazi na watu tofauti unapata uelewa mpya kutoka kwa watu hao ambao mwanzo jambo hilo ulikuwa hulifahamu.
6. Wekeza kwenye miradi ya muda mrefu: mwandishi Thiel anasisitiza kuwa ili uweze kupata mafanikio basi jifunze kuweza kwenye miradi ya muda mrefu kwa sababu ukiwa na miradi ya muda mfupi utakuwa unatafuta mafanikio ya haraka kitu ambacho kitafanya mafanikio hayo yasidumu pia. Ili uweze kufanikiwa kwenye miradi ya muda mrefu basi hakikisha unafanya vitu kwa mwendelezo bila kuchoka.
7. Jifunze kutatua matatizo: dunia ya sasa imejaa changamoto nyingi sana, pamoja na changamoto hizo basi jifunze kupata ufumbuzi wa changamoto hizo, ukifanikiwa kwenye hilo itakuwa ndiyo njia nzuri ya kutoka sifuri hadi moja kama jina la kitabu linavyosema.
8. Jifunze kusimamia mabadiliko: inaelezwa kuwa uvumbuzi huleta mabadiliko na huo ndiyo ukweli. Ukiwa mvumbuzi basi jiandae kupata mabadiliko. Unapofanya uvumbuzi fulani jiandae pia jinsi ya kusimamia mabadiliko hayo ili uweze kuendelea mbele na hatimaye upate mafanikio uyatakayo.
9. Wekeza kwenye kujifunza: mwandishi Thiel anasisitiza sana suala la kujifunza kwa sababu unapojifunza unajua mengi zaidi. Pia anasema unapojifunza kunakusaidia sana kukua kimawazo, ambapo mawazo hayo yatakusaidia kuweza kupata mafanikio uyatakayo.
Kumbuka, kila mmoja anaweza kupata mafunzo tofauti kutoka kwenye kitabu hicho, lakini hizi ni baadhi tu ya dhana kuu ambazo nimezitoa kwenye kitabu hicho.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya
.jpeg)
0 Comments